
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomez Da Rosa.
Gomez amesema, “Kwanza tuweke pembeni ligi ya mabingwa, yaliyopita yamepita, tumefuzu robo fainali na tutatcheza mwezi ujao na tun amuda wa kujiandaa. Sasa tunataka kuelekeza ngucu kwenye Ligi, ni lengo letu kuu”.
“Lazima tuchukue nafasi ya kwanza haraka na natumaini tutfanya hivyo kwenye hii michezo minne, ni muhimu sana na kuwekeza nguvu kwenye hilo kwasababu tunataka kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika kila mwaka”.
“Natarajia utashi na hamasa kubwa na nitacheza na wachezaji wangu bora kabisa” Gomez akamalizia.
Simba inataraji kujitupa dimbani siku ya kesho Aprili 14, 2021 saa 1:00 usiku kwenye dimba la Mkapa kuanza kucheza michezo yake ya kiporo baada ya kukamilisha michezo ya hatua y amakundi ya klabu bingwa Afrika.
Kuelekea kwenye mchezo huo, nae kocha wa msaidizi wa Mtibwa Sukari, Vincent Barnabas amesema licha ya ubora walionao Simba lakini wamejipanga vilivyo kuwakabiri na mkuondoka na matokeo mazuri.
“Simba nadhani ni kati ya timu bora Afrika, ni timu amabyo inacheza vizuri kwa pamoja lakini tutajipanga tuone ni namna gani tunaweza kuwakabiri.”
“Utakuwa mchezo wa kufunguka zaidi, timu zote zinacheza hivyo watu wategeme mchezo mzuri”.
Simba ipo nafasi ya tatu, ikiwa na alama 46 baaada ya kucheza michezo 20 michezo 4 nyuma ya kinara Yanga mwenye alama 51, utofauti wa alama 5 huku Azam ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 47 baada ya kucheza michezo 25.