Jumatano , 23rd Jun , 2021

Chama cha mchezo wa Tenisi nchini Serbia, kimesisitiza kwamba mchezaji wao Novak Djokovic atashiriki michuano wa Olimpiki inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Japan.

Novak Djokovic akiwajibika uwanjani

Kinara huyo katika viwango vya ubora Duniani ambaye ndiye bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa iliyohitimishwa hivi karibuni anadaiwa kutaka kujiondoa kufuatia kupata maumivu ya mgongo.

Kumekuwa na wimbi la nyota kadhaa kutangaza kujiondoa katika michuano hiyo na siku za hivi karibuni Rafael Nadal ni mmoja ya mastaa hao waliojiondoa katika michuano hiyo.

Nyota mwingine kwa upande wa wanawake ambaye alitangaza kutoshiriki michuano hiyo ni Naomi Osaka hivyo kupelekea kuondoa mvuto kwa kiasi fulani katika michuano hiyo.