Novak Djokovic akionyesha makeke yake
Mapema wiki hii, mkuu wa Australian Open, Craig Tiley alisema kuwa baadhi ya wachezaji ambao hawajachanjwa wameruhusiwa kucheza katika Grand Slam ya kwanza ya mwaka huu.
Djokovic, mshindi mara tisa wa Australian Open, hajazungumza hadharani kuhusu hali yake ya chanjo kuelekea kwenye mashindano hayo yanayoanza tarehe 17 Januari mwaka kwenye mji wa Melbourne.
Wachezaji na wafanyakazi wote watakaoshiriki kwenye mashindano hayo, lazima wapewe chanjo au wapate msamaha unaotolewa na jopo huru la wataalamu wa michuano hiyo.
