
Kipindi cha 'Kipenga Xtra' kinampa nafasi msikilizaji ya kusikiliza mjadala wa siku kupitia kipengele cha 'Kali ya Siku' ambapo kunakuwa na mada inayohusu habari kubwa katika tasnia ya michezo kitaifa ama kimataifa.
Katika 'Kipenga Xtra' wasikilizaji pia wanapata nafasi ya kuhusika kwenye kipindi kupitia kupiga simu na kutoa maoni yao juu ya mada ya siku husika kupitia kipengele cha 'Ngenga za Kitaa'.
Pia kuna kipengele cha 'Nani kapata nani kakosa', ambacho kinahusisha msikilizaji kupiga simu na kujibu swali la kimichezo linalokuwa limeandaliwa kwa siku husika na akishinda anapata zawadi.
Kabla ya kipindi cha kufika tamati msikilizaji anapata taarifa mpya za kimichezo kupitia Kipengele cha 'Dakika za Nyongeza'. Kipengele hiki kinahabarisha habari za kitaifa na kimataifa.