
Winga wa Azam FC, Farid Mussa Malik ambaye yupo nchini Hispania kwenye majaribio
Farid ambaye ameshafanya majaribio kwa siku tatu katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili ijulikanayo kama Segunda ya nchini Hispania amesema, katika majaribio ambayo alipewa kwa kucheza mechi alicheza vizuri na kocha alikubali kiwango chake.
Farid amesema, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa majaribio Kocha alimpa maelekezo na marekebisho kwa makosa aliyoyaona yeye na anaamini kwa uelewa pamoja na uwezo wake utaweza kumfikisha mbali.
Farid amesema, soka la Hispania lipo vizuri kwa jinsi alivyoliona kwa kipindi kifupi na katika masiha yake alikuwa na ndoto za kucheza soka la nchini Hispania.
Mara baada ya kumaliza majaribio na timu ndogo ya Tenerife, wiki ijayo anaendelea na timu kubwa ya Tenerife na baada ya hapo atapelekwa katika timu za Las Palmas au Malaga ambazo zinashiriki Ligi kuu nchini humo.
Farid amefanyiwa vipimo vya Moyo hii leo na kesho Alhamisi majibu yanatarajiwa kutoka na baada ya hapo mustakabli wake zaidi utajulikana.