Jumanne , 28th Jun , 2016

Klabu ya soka ya Azam FC imesema haikuwa na lengo la kukataa ofa ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Farid Musa Maliki ambaye amefuzu majaribio katika timu ya ligi daraja la kwanza nchini Hispania Derpotivo Tenerlife na kumpeleka kwa mkopo

Kiungo wa Azam FC na Taifa Stars Faridi Musa akiwa nchini Hispania.

Klabu ya soka ya Azam FC imesema ililazimika kufanya maamuzi ya kumpeleka kwa mkopo mshambuliaji huyo chipukizi wa timu hiyo na Taifa Stars Farid Musa ambaye amefuzu majaribio na timu ya Diportivo Tenerife ya Hispania.

Afisa habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga amesema uamuzi huo umetokana na kiasi kidogo cha pesa ya usajili ambayo Wahispania hao walitaka kuwalipa ili kunasa saini ya chipukizi huyo mwenye kipaji kikubwa ambaye amekulia katika kituo cha soka la vijana [akademi] ya timu hiyo maeneo ya Chamazi jijini Dar es Salaam.

Aidha, Jafar amesema uamuzi huo pia umezingatia maslai ya klabu kwani kama wangeamua moja kwa moja kumuuza kwa bei chee kama walivyotaka Wahispania hao kwa mujibu wa ofa yao basi wao waliomlea kwa gharama kubwa wasingeona faida ya mauzo ya mchezaji huyo zaidi ya kupata sifa ya kutoa mchezaji anayecheza ligi kubwa barani Ulaya.

Akimalizia umauzi wa kumtoa kwa mkopo mchezaji Farid Musa, amesema utawanufaisha wao kwa kiasi kikubwa kama mchezaji huyo akipata timu kubwa tena ya daraja la juu katika sehemu yoyote itakayolizika na uwezo wake basi ni wazi mauzo yake yatakuwa ya juu na hata mgawo wa mauzo hayo utakuwa katika asilimia ambayo itakidhi gharama za klabu hiyo na faida kidogo.