Jumanne , 11th Feb , 2020

Shirikisho la Soka Duniani FIFA na umoja wa wachezaji FIFPRO unaandaa mfuko utakaosaidia kuwalipa wachezaji wasio na mishahara na wale ambao hawapati mishahara pindi klabu zao zinapopitia changamoto za kiuchumi.

Makao makuu ya FIFA

Hiyo imekuja kufuatia muendelezo wa klabu nyingi duniani kuporomoka kiuchumi, ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jumla ya klabu 20 duniani zimeanguka kiuchumi na kukwamisha mamia ya wachezaji.

Mfuko huo utazisaidia kulipa mishahara klabu klabu zilizoporomoka kiuchumi huku zikiwa zinafanya biashara ili zirejee katika hali yake.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema ametenga kiasi cha Pauni Milioni 12.3 kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji ambao hawatalipwa na klabu zao kuanzia 2020 hadi 2022 huku takribani Pauni Milioni 3.8 zikitengwa kuwalipa wachezaji ambao hawajalipwa kuanzia 2015 hadi 2020.

"Makubaliano kati yetu na washirika wetu ni kuwasaidia wachezaji walio katika mazingira magumu na kazi yetu ni kuonesha uwepo wetu kama chombo kinachoongoza mpira", amesema Infantino.