Frank Domayo apelekwa South Afrika kutibiwa

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Mchezaji wa Timu ya Azam FC, Frank Domayo, ameelekea Afrika Kusini alfajiri ya leo, kwa ajili ya matibabu ya tatizo la kuchanika msuli wa nyama ya paja

Mchezaji wa Timu ya Azam FC, Frank Domayo.

Taarifa ya Klabu ya Azam FC, imesema matibabu yake yatachukua muda wa siku 10, ambapo anaenda kutibiwa katika Hospitali ya Vincent Palotti chini ya Dr. Robert Nickolas.

Domayo alipata majeraha hayo, wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON, dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Domayo ameambatana na Daktari wa timu, Dkt. Mwanandi Mwankemwa.