Fulham nayo yaenda na maji EPL

Jumanne , 11th Mei , 2021

Klabu ya soka ya Fulham inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza, imekamilisha orodha ya timu tatu zinazopaswa kushuka daraja katika msimu huu.

Kocha wa Fulham Scott Parker

Fulham iliruhusu kufungwa 2-0 na Burnley usiku wa jumatatu katika uwanja wake wa nyumbani Craven Cottage, matokeo yanayowafanya washuke rasmi daraja akiungana na Sheffield United na West bromwish Albion.

Pamoja na kubakiza michezo 3 kumaliza msimu ,hata kama watapata kushinda na kupata alama zote tisa haitaweza kubadili msimamo kwa kuwa timu ya juu yao kwa maana ya Southampton ina alama 10 zaidi.

Fulham inayofundishwa kwa sasa na kocha kijana Scott Parker imekuwa na historia ya kupanda na kushuka, kwa misimu mitatu hii, imeshuka mara mbili msimu wa 2018/2019 ikacheza 'championship'kwa msimu moja 2019/2020 ikapanda tena imecheza msimu wa 2020/2021 imeshuka tena

Licha ya kuwa na nyota kibao katika kikosi chao kama Aleksandar Mitrovic, Andre Frank Zambo Anguisa, Mario Lemina ,Ademola lookman na Ruben loftus Cheek,imeshuka ikiwa na takwimu hizi michezo 35 alama 27 hadi sasa ushindi mara 5 sare 12 kupoteza 18 magoli ya kufunga 25 ya kufungwa 27