"Hakuna kombe wala mechi ndogo kwetu, kila michuano tunaichukulia kwa uzito ule ule kwasababu ili kuwa klabu kubwa na yenye historia kubwa kama Liverpool na United ni lazima ushinde mataji mengi uwezavyo hivyo tutajitahidi kushinda mchezo wetu dhidi ya Bristol City'', amesema Pep.
Guardiola ameongeza kuwa pamoja na kupata matokeo mazuri msimu huu lakini ni lazima wamalize kwa kushinda mataji mengi kadri inavyowezekana kwani matokeo au kucheza vizuri hayana mana kama mwisho wa msimu hautachukua vikombe.
Guardiola ambaye amewahi kufundisha klabu za Barcelona na Bayern Munich amesisitiza kuwa kamwe hawezi kuangalia mechi zijazo kwani ni makosa makubwa. ''Kwenye soka ni muhimu kuangalia mechi unayoenda kucheza sio mechi zijazo'', amesema.
Manchester City ina alama 62 kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini England ikiwa ni alama 15 juu ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili kwa alama 47.







