
Erling Haaland kafunga mabao 9 kwenye michezo 5 ya EPL
Mabao hayo yamemfanya Haaland afikishe mabao 9 kwenye michezo 5 ya EPL ikiwa ni idadi kubwa ya mabao kuwahi kufungwa na mchezaji mmoja kwenye ligi hiyo kwenye michezo 5 ya awali. Hii pia ni Hat trick ya pili anafunga kwenye EPL tangu ajiunge na Manchester City.
Hat-trick hizo mbili zimemfanya Halaand afikie idadi sawa ya Hat trick na wachezaji kama Eden Hazard amabye alicheza Chelsea, Sadio Mane mchezaji wa zamani wa Liverpoon na Heung-Min Son wa Tottenham. Takwimu pia ziaonyesha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao hayo 9 akiwa amegusa mpira mara 101 tu.
Mabao mengine ya Manchester City kwenye mchezo huo yamefungwa na Joao Cancelo na Julian Alvarez. Kwa ushindi huu City imefikisha alama 13 ikiwa nafasi ya pili tofauti ya alama 1 dhidi ya vinara wa Ligi Arsenal wenye alama 15.