
(Nyota Lewis Hamilton na Serena Williams wakiwa kwenye picha ya pamoja)
Hamilton ambaye ni bingwa mara saba wa dunia wa michuano ya langalanga sambamba na Serena Williams ambaye ametwaa mataji 23 ya Grandslam kwenye mchezo wa tennis wanaungana na rais wa chama cha riadha duniani Sebastian Coe ambaye anamuunga mkono tajiri Sir Broughton
Broughton pia anaungwa mkono na wamiliki wenza wa klabu ya Crystal Palace Josh Harris na David Blitzer huku akipata msaada mkubwa wa kifedha kutoka kwa wawekezaji wengine kama Michael Klein na Lord Coe huku Hamilton na Serena Williams hawatahusika na maamuzi yoyote kwenye mambo ya soka iwapo tenda ya Sir Broughton itashinda dili la kuinunua klabu ya Chelsea .