
Akizungungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Stephen Ally amesema, mchezaji huyo ameondoka bila ruhusa na baadaye walisikia akilalamika kuwa hajapangiwa nyumba suala lililochangia kuondoka na kurundi nyumbani kwao.
Ally amesema, suala hilo lipo kinyume na sheria la Klabu hiyo na suala la yeye kupangiwa nyumba alitakiwa kuwasiliana na uongozi na sio kuondoka kama alivyofanya.