Jumanne , 8th Dec , 2020

Ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya makundi msimu huu wa 2020-21 itakamilishwa usiku wa leo Disemba 08 na kesho Disemba 09 2020, ambapo mpaka hivi sasa jumla ya timu 9 zimeshafuzu hatua ya 16 bora na timu 13 zinawania nafazi 7 zilizobaki.

Wanafainali wa lUCL msimu uliopita PSG, wakiongozwa na Neymar (Kushoto), Kylian Mbappe (Katikati) na Angel di Maria (Kulia) watakuwa na kibarua cha kuhakikisha wanashinda leo ili wafuzu hatua ya 16 bora.

Timu zilizofuzu hatua ya mtoa yani 16 bora ni mabingwa watetezi Bayern München kutoka kundi A, Manchester City na FC Porto kutoka kundi C, Liverpool kutoka kundi D, Chelsea na Sevilla kutokoka kundi E, kundi F ni Borusisia Dortmund pekee, Juventus na Barcelona nazo zimefuzu kutoka kundi G.

Ni makundi mawili tu ndio ambayo bado hayajatoa timu iliyofuzku hatua ya 16 bora, makundi hayo ni kundi B lenye timu za Mönchengladbach, Shakhtar Donetsk, Real Madrid, na Inter, kundi jingine ni H linaloundwa na timu za Manchester United, Paris Saint-Germain, Leipzig na İstanbul Başakşehir.

Vita kubwa inayosubiriwa na wengi ni kuona katika nafasi 7 zilizobaki ni timu zipi zitaenda na ni jumla ya timu 13 zinawania nafasi hizo 7.

Timu hizo ni Atlético Madrid, Rb Salzburg, Borussia Mönchengladbach, Shakhtar Donestk, Real Madrid, Inter Milan, Atalanta, Ajax, Lazio, Club Brugge, Manchester United, Paris Saint-Germain, na RB Leipzig.

Haya ni mahitaji ya kila timu miongoni mwa timu zenye nafasi ya kufuzu ili iweze kufuzu hataua ya 16 bora miongoni mwa timu hizi 13 zinazowania nafasi hizo 7 zilizobaki.

Kundi F, kwenye kundi hili Dortmund wameshafuzu nafasi imebaki wa Lazio na Club Brugge ambao wanakutana wao kwa waona tofauti yao ikiwa ni alama 2, Lazio wapo nafasi ya 2 wakiwa na alama 9, wakati Brugge wana alama 7 nafasi ya 3.

Lazio watafuzu hatua ya 16 bora endapo kama watashind au watapata sare katika mchezo huu wakati Club Brugge wanahitaji ushindi ili wafuzu hatua hiyo.

Kundi H, timu 3 kutoka kundi hili zote zinanafasi ya kufuzu Manchester Utd wanaongoza kundi wakiwa na alama 9 sawa na PSG walio nafasi ya 2 na RB Leipzing walio nafasi ya 3.

Rb Leipzig wanaminyana na Man United, Manchester United watafuzu hatua ya 16 bora endapo kama wataepuka kufungwa kwenye mchezo huu, wanahitaji sare au ushindi, wakati Leipzig wanahitaji ushindi au kama wasiposhinda basi watahitaji PSG wafungwa au watoke sare dhidi ya İstanbul Başakşehir,

PSG watafuzu endapo kama wataepuka kichapo mbele ya İstanbul Başakşehir, au kama wakifungwa basi mchezo wa Man United na Leipzig usimalizike kwa sare.

Kundi A, ndilo lenye bingwa mtetezi Bayern Munich na ameshafuzu hatua inayofata, hivyo nafasi inayowaniwa ni moja tu ambapo vita ni ya Atlético Madrid na RB Salzburg na kikubwa wanaumana wao kwa wao kwenye mchezo wa mwisho ambapo Salzburg ni wenyeji wa Atletico.

Tofauti yao ni alama 2, Atletico wapo nafasi ya 2 kwenye kundi wakiwa na alama 6 ikiwa ni tofauti ya alama 2 dhidi ya Salzburg wenye alama 4 walio nafasi ya 3.

Wenyeji Salzburg wanahitaji ushindi pekee ili wafuzu hatua ya 16 bora, wakati ushindi au Sare itatosha kuwavusha Atletico Madrid.

Kimbembe kipo Kundi B, timu zote 4 kwenye kundi hili zina nafasi ya kufuzu lakini zinahitajika timu 2 tu.

Kwa sasa msimamao wa kundi hilo ulivyo timu inayoongoza kundi ni Borussia Mönchengladbach wenye alama 8, nafasi ya pili Shakhtar wana alama 7 nafasi ya 3 ni Real Madrid wakiwa na alama 7 na Inter Milan ndio wanaburuza mkia wakiwa na alama 5.

Monchengladbach itafuzu ikiwa wataepuka kufungwa na Real Madrid, au kama Shakhtar itatoka sare na inter Milan pia Manchengladbach watamaliza vinara wa kundi kama watashinda.

Shakhtar watapita kama wataifunga Inter Milan au kama michezo yote ya kundi hili itamalizika kwa sare.

Mabingwa wakihistoria Real Madrid wanahitaji ushindi dhidi ya Mönchengladbach, ili kujihakikishia nafasi hatua ya 16 bora, au kama wakipata sare basi Shakhtar wafungwe na Inter.

Vijana wa kocha Antonio Conte Inter itapita endapo kama wataifunga Shakhtar, na mchezo wa Real Madrid na Mönchengladbach usimalizike kwa sare.

Kundi D, nafasi iliyobaki ni 1 kwani tayari Liverpool washafuzu kutoka kwenye kundi hili, hivyo nafasi moja iliyosalia inawaniwa na Atalanta na Ajax ambao wanatofautiana kwa alama 1, Atalanta wana alama 8 wapo nafasi ya 2 wakati Ajax wana alama 7 nafasi ya 3.

Hawa nao wanapunguzana wenyewe kwani wanakutana katika mchezo wa mwsiho wa kundi hili,
Atalanta watafuzu endapo kama wataepuka kufungwa na Ajax hivyo hata matokeo ya sare yatatosha kuwavusha.

wakati Ajax wanahitaji ushindi tu wa alama zote 3 ili watinge hatua ya inayofata ya 16 bora.