
Timo Werner (kushoto) na Thomas Tuchel (kulia).
Tuchel ameyasema hayo leo wakati Chelsea inajiandaa kucheza na West bromwich Albion kwenye EPL na kumataza nyota huyo wa kijerumani kuacha kufanya mazoezi ya kufunga na badala yake acheze bila uoga.
“Nimemwambia, hauhitaji kufanya hivyo. Mwili wako, akili yako vinajua namna ya kufunga. Umefanya hivyo tokea ukiwa na umri wa miaka 6. Kwahivyo usijali, mabao yatakuja tu. Kitu kizuri cha kufanya hivi sasa ni kuganya kazi kwa juhudi kubwa na kucheza bila kuogopa”.
Tuchel pia amejibia suala la nyota wake huyo kukosa nafasi ya wazi kwenye hususani hivi karibuni kwenye mchezo wa timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Macedonia ya Kaskazini dakika za lala salama na hatimaye Ujerumani ikapoteza mchezo kwa 2-1 dakika chache baada ya Werner kukosa nafasi hiyo.
(Werner akikosa nafasi ya wazi kwenye mchezo dhidi ya Macedonia Kakazini kwenye mchezo ambao Ujerumani walipoteza mabao 2-1.)
“Alikosa nafasi na sasa kila mtu anamuongelea kitu ambacho kinanishangaza. Ukweli ni kwamba hakuanza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya tatu , kwahiyo huenda alipata dakika chache angepata nyingi huenda angefunga bao”.
“Ni uamuzi mwepesi sana kumnyooshea kidole Timo, kitu ambacho siwezi kukielewa na kukikubali. Nina furaha amerejea Chelsea kwasababu hapa analindwa. Tunahitaji mengi kutoka kwake na hapa tunapata mengi kutoka kwake”.
“Ndiyo, yupo kwenye kipindi ambacho hajiamini. Lakini anajituma zaidi kwa ajili ya timu. Anatufungia mabao, anatengeneza nafasi za mabao, ana faida ya kusaidia timu kupata penalti. Kwahiyo kama kipindi hiki ni kigumu kwake na bado anafanya haya naweza kukubali na ni kitu kizuri”.
Maneno ni dhahiri kocha huyo anamkingia kifua mshambuliaji wake ili apunguzee presha na kumtibu kisaikolojia aweze kuwa mtulivu na kurudisha hali ya kujiamini ambayo kwa sasa ameipoteza.
Werner amefunga mabao 10 na kutengeneza mabao 10 kwenye michezo 39 aliyoichezea Chelsea kwenye michuano yote msimu huu, lakini akiwa na mabao 5 na kutengenza mabao 8 kwenye michezo 28 ya EPLpekee.