
Mashabiki wa The Reds wamepokea habari hii kwa hisia mseto, hasa baada ya kutambulishwa kwa uzi mpya wa Adidas ambao wengi wamesema “ni moto wa kuotea mbali.”
Rangi nyekundu safi ya jadi, ikikamilishwa na mistari mitatu ya Adidas mabegani, inakumbusha enzi za utukufu wa Liverpool wa miaka ya nyuma. Ubunifu wa kisasa unadumisha heshima ya Anfield huku ukituma ujumbe wa matumaini mapya kwa msimu ujao.
Jezi Hii Ni Ya Makombe au Fashion Tu?
Hili ndilo swali linalotawala midomoni mwa mashabiki: je, Adidas wataleta bahati kama ya zamani? Au jezi hii itasalia kuwa tu kivutio cha macho na mitindo mitandaoni?