
Picha ikionesha baadhi ya matukio katika mchezo wa usiku wa jana ambapo Liverpool aliifunga RB Leipzig 2-0.
Klopp ameyasema hayo baada ya Liverpool kufuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-0 huku ikishinda mabao 2-0 kwenye kila mchezo na wwashambuliaji wake Mohamed Salah na Sadio Mane wakifunga mabao mawili mawili na kuiondosha Leipzig.
Klopp amesema “Hatupo vizuri kwa sasa, huu sio ule msimu unaofananania na sisi kubeba kombe hili. Tunapaswa kusubiri droo, na itakuwa ngumu sana kwa yeyote tutakayepangwa naye. Kwasasa hatufikirii sana huko, tunafikiria siku ya kesho na kuhusu Wolves tutakaocheza nao siku ya jumatatu.”
“Tunamwendo na ari nzuri kwenye michuano hii lakini ari hii bado hatuna kwenye michezo ya ligi kuu, na tunamichezo ya kutusaidia kuturudisha kwenye ari yetu na hiyo bila shaka, itatusaidia kweney michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya”
Maneno hayo ni dhahiri kuwa kocha wa majogoo hao wa jiji wanakiri kutokuwa kwenye kiwango bora cha ushawishi wa kuweza hata kubeba kombe la ligi ya mabingwa barani humo.
Ikumbukwe kuwa, Liverpool ilicheza fainali mbili mfululizo na kubeba kombe hilo mara ndani ya misimu mitatu iliyopita.
Droo ya Liverpool kukipiga na nani kwenye hatua ya robo fainali na droo ya nusu fainali inataraji kupangwa tarehe 19 mwezi huu.