
Akizungumza jijini Dar es salaam, Kaijage amesema, walitakiwa kuondoka leo hii kuelekea visiwani humo lakini imeshindikana kutokana na muingiliano wa ratiba hivyo timu hiyo itaendelea na maandalizi ikiwa jijini dar es salaam.
Kaijage amesema, kikosi hicho kimerudi kambini ambapo hapo awali kilikuwa katika mapumziko ili kuweza kukamilisha zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupigia kura na hivi sasa kikosi chote kimewasili kambini na kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba nne mwaka huu nchini Congo Brazzaville.