
Kipande cha picha kushoto, kinaonesha namna Harry Kane alivyopata maumivu kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia baada ya kuangukiwa na Richarlson.
Mashaka hayo yanakuja baada ya mshambuliaji huyo tegemezi kikosini humo kupata maumivu ya kifundo cha mguu kwenye mchezo dhidi ya Everton juma lililopita mpaka kupelekea nyoya huyo kushindwa kufanya mazoezi ya jana ya pamoja na wachezaji wenzake.
Kane ambaye ni kinara wa upachikaji mabao kwenye ligi kuu England kwa sasa akiwa na mabao 21 pamoja na kuwa kinara wa kutengeneza nafasi za mabao akiwa ametengeneza mabao 13, atalazimika kufanyiwa vipimo dakika za mwisho kuona kama ataweza kuwa fiti kuingia dimbani.
Mchezaji mwingine wa Spurs aliyethibitishwa kukosekana ni mlinzi wa kushoto Ben Davies ambaye pia anasumbuliwa na kifundo cha mguu.
Kwa upande wa Manchester City wamethibitisha kuwa, mgungaji bora wa muda wote klabuni hapo, Sergio Aguero na kiungo Kevin Debruyne wamerejea kikosini na wananafasi kubwa ya kucheza mchezo huo ilhali John Stones akikosekana kutoka na kuoneshwa kadi mchezo uliopita.
Hii itakuwa ni fainali ya tatu kwa Spurs tokea itwae taji hilo mwaka 2008 ilipoifunga Chelsea mabao 2-1 chini ya kocha Juande Ramos huku mwaka 2009 wakipoteza mbele ya Manchester United na mwaka 2015 wakilipiziwa kisasi kwa kufungwa na Chelsea.
Na kama Manchester City itafanikiwa kutwaa kombe hilo basi wataweka rekodi sawa na klabu ya Liverpool ya kutwaa kombe hilo mara nne mfululizo tangu mwaka 1981 hadi 1984 wakati ambao Ryan Mason kocha wa muda wa Spurs kwasasa utakuwa ni mchezo wake wa pili.