Katibu Mkuu wa TFF afika ofisi za TAKUKURU

Jumanne , 19th Mei , 2020

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Kidao Wilfred leo Mei 19, 2020 amefika katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Kidao Wilfred

Hivi karibuni Mkurugenzi wa TAKUKURU Brig. John Mbungo aliweka wazi kuwa wanaendelea kuwahoji watu mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali.

East Africa Television na East Africa Radio, zimefika makao Makuu ya TAKUKURU ili kujua kinachoendelea, lakini baada ya kutoka ndani Katibu Mkuu Kidao Wilfred hakutaka kuongea chochote.

Tunafanya juhudi za kuongea na Mkurugenzi wa TAKUKURU Brig. John Mbungo ili kujua zaidi.

Endelea kufuatilia mitandao yetu tutakupa taarifa zaidi.