
KCCA juu na Mtibwa Sugar chini
Akiongea katika mkutano na wanahabari leo, makao makuu ya TFF, kocha wa KCCA, Mike Mutebi, amesema pamoja na kutafuta matokeo lakini watacheza soka la kuburudisha.
''Tunajua Mtibwa ni timu ngumu lakini nafikiri changamoto watakayotupa tunaimudu hivyo tutajaribu kucheza kwa kutoa burudani zaidi na kutafuta ushindi ili tusonge mbele'', amesema Mike.
Naye kocha wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila amekiri kuwa mlima ni mkubwa lakini watajitahidi kuweza kutumia vizuri nafasi watakazopata ili waweze kufunga mabao mengi zaidi.
Mechi ni ngumu, katika mchezo wa kwanza tuliruhusu mabao 3-0 hivyo tuna kazi kubwa ambayo tumejiandaa kuifanya ili tupate matokeo yatakayo ruhusu tusonge mbele na nina amini hilo linawezekana wachezaji wakijituma.
Mtibwa inahitaji kufunga mabao 4-0 ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho barani Afrika. KCCA wao wanahitaji sare yoyote au wasifungwe zaidi ya mabao 2.