
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane.
Kauli hiyo inakuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu Kane agusie kuwa angeihama klabu hiyo iwapo hatofanikiwa kutwaa mataji na kwa mwenendo wa Tottenham Hotspurs wa kusuwasuwa zipo dalili za nyota huyo kutimka mwishoni mwa msimu huu.
(Nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Roy Keane.)
Keane ambaye kwasasa ni mchambuzi wa moja ya kitua mashughuli cha michezo nchini Uingereza, amemtaka Kane kuamua mapema ili atengenezea heshima yake kwa kutwaa mataji akiamini kwamba kwa umri wa miaka 27 alionao hana muda wa kusubiri zaidi ya msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza ambaye ameifungia Spurs mabao 160 katika ligi kuu, amekuwa akihusishwa na klabu za Manchester United, Manchester City na Real Madrid lakini bado ana mkataba wa miaka mitatu na klabu yake ya sasa.