Jumanne , 29th Dec , 2020

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na michuano ya timu za taifa kwa  wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika 'CHAN', kimewekwa wazi na TFF baada ya kuchaguliwa na benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na kocha mkuu Etiene Ndayiragije.

Kocha Mkuu Etiene Ndayiragije (kulia), na kocha msaidizi Selemani Matola (kushoto)

Kikosi hicho kilichotajwa jioni ya leo Disemba 29, 2020, kinatazamiwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya michuano hiyo tarehe 1, Januari 2021 na kutaraji kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Baadhi ya wachezaji ambao hawajaitwa kwenye kikosi hicho ni mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein, kiungo Jonas Mkude wa Simba, Mlinda Mlango David Kissu, Kiungo Salum Aboubakari na Mudhatir Yahya wa Azam.

Ikumbukwe kuwa michuano ya CHAN inatazamiwa kuanza Januari 16 hadi Februari 7 mwaka 2021 nchini Cameroon.

Soma kikosi kamili hapo chini