
Wenger
Wenger anatarajiwa kumaliza mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa msimu huu, na ameshapewa nyongeza nyingine ya miaka miwili lakini Mfaransa huyo bado hajatangaza kama ataendelea klabuni hapo.
Arsenal ipo nafasi ya sita na inatakiwa itafute pointi saba kuingia nafasi ya nne, huku ikiwa imebaki na michezo nane.
"Nimeiongoza Arsenal kwa zaidi ya michezo 1,100 na hatujazoea kupoteza kama hivo," alisema Mfaransa huyo.
"Tunatakiwa kujibu haraka sana na tusikubali hili."
Baadhi ya mashabiki waliosafiri na timu hiyo, walimwambia Wenger ulikuwa ni "muda wa kuondoka".