Jumatano , 2nd Nov , 2016

Meneja wa Sunderland David Moyes amepigwa marufuku mechi moja na faini ya pauni 8,000 na Chama Cha Soka cha England kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya mwamuzi wa mechi.

David Moyes

 

Kisa hicho kilitokea baada ya mwamuzi kuinyima Sunderland mkwaju wa penalti katika dakika ya 90 ya mechi ya Jumatano wiki iliyopita ambapo klabu hiyo ilishindwa 1-0 na Southampton katika Kombe la FA.

Baada ya mechi hiyo, Moyes alisema tatizo lilitokea alipoandamwa hadi pahala alipokuwa amesimama, hivyo  alitumia lugha ya matusi.