
Kocha mpya wa Azam FC Denis Lavagne
Kocha huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 58 alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Azam FC usiku wa kuamkia leo na anakuja kuchukua mikoba ya kocha Abdihamid Moallin aliyefutwa kazi katika nafasi hiyo Agosti 29, 2022.
Lavagne ana uzoefu na soka la Afrika, amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Cameroon kati ya mwaka 2011 hadi 2012 lakini pia amefundisha vilabu kadhaa vikubwa Afrika ambavyo ni Etoile Du Sahel, Smouha, Coton Sports, Al Hilal, USM Alger na JS Kabylie.
Mafanikio yake makubwa katika soka la Afrika ni pale alipokiongoza kikosi cha JS Kabylie ya Algeria kucheza fainali ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca ingawa alipoteza mchezo huo kwa mabao 2-1.