
Mchezo huo wa mwisho wa kundi A, unapigwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe saa 9 alasiri kwa saa za Africa Mashariki.
“Tunahitaji kushinda mchezo huu na tunautilia uzito ili tumalize salama na kujiwekea rekodi ya kipekee,” alisema.
Wawakilishi hao wa Tanzania walitupwa rasmi kwenye michuano hiyo baada ya Medeama ya Ghana kuifunga Mazembe mabao 3-2 na hivyo kufikisha pointi nane ambazo Yanga haiwezi kuzifikia hata ikishinda mechi ya leo.
Licha ya kutolewa, lakini Yanga hawajakwenda Congo DR, kukamilisha ratiba bali wanataka kushinda ili kuleta heshima na sifa ya kumaliza japo na pointi 7.