Jumatatu , 13th Jul , 2015

Kocha wa Timu ya Toto Africa ya Mwanza John Tegete amesema leo anatarajia kuweka wazi kikosi chake atakachoingia nacho kwenye kwenye Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22 mwaka huu.

Katika taarifa yake, Tegete amesema, baada ya mazoezi ya wiki iliyopita wanatarajia kufanya mchujo wa wachezaji katika kikosi hicho kwa kukusanya wachezaji wenye uwezo.

Tegete amesema, wapo wachezaji wengi kwenye kikosi hicho ambao walikuwa katika majaribio hivyo wanahitaji kuwafanyia mchujo baada ya kuona viwango vyao.