Kombe la EPL ladondoshwa kutoka juu ya basi

Jumanne , 21st Mei , 2019

Hapo jana, Mei 21, klabu ya Manchester City ilifanya sherehe kubwa kwa timu za wakubwa za wanaume na wanawake kusheherekea mataji waliyoshinda msimu huu.

Man City wakiwa katika basi na moja ya mataji yao

Klabu ya wanaume ya Man City ilikamilisha taji la tatu la ndani wikiendi iliyopita kwa kuifunga Watford jumla ya mabao 6-0 katika fainali ya kombe la FA, mataji mengine iliyoshinda ni la Ligi Kuu nchini Uingereza EPL na kombe la ligi 'EFL'. Timu ya wanawake ikishinda kombe la FA.

Katika video moja iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, imemuonesha mshambuliaji wa klabu hiyo, Sergio Aguero akijilaumu baada ya kulidondosha taji la EPL kutoka juu ya basi walilokuwemo, lakini baadaye lilirudishwa tena.

Sambamba na sherehe hiyo, Manchester City ilimtangaza kiungo, Bernardo Silva kuwa mchezaji bora wa msimu wa klabu hiyo kwa msimu wa 2017/18.