Kuhusu Yanga kuwa na mgogoro, Mwenyekiti ajibu

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla, amesema yeye hana tofauti na makamu wake Frederick Mwakalebela kama ambavyo imekuwa ikielezwa mtaani.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla.

Akiongea na EATV & EA Radio Digital, Msolla amesema wananchama wa Yanga wanatakiwa kupuuza uvumi huo kwasababu wao wako vizuri na wanafanyakazi kwa kuendeleza klabu.

'Wale ni watu wachache wahuni, sisi kama uongozi na klabu kwa ujumla tupo pamoja, ila tu tunavyo vipaumbele katika matumizi ya fedha kwahiyo wachache waliokuwa wananufaika na pesa za klabu lazima waumie', amesema.

Msola ameongeza kuwa kuhusu madeni pamoja na matumizi ya fedha, wamejiwekea malengo ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, ambapo kwasasa wamejikita kuhakikisha timu inasafiri vizuri kwenye mechi za kimataifa ili ifanye vizuri.

Jana Oktoba 6, 2019 klabu ya Yanga ilifanikiwa kupata alama tatu za kwanza kwenye ligi kuu baada ya kuifunga Coastal Union goli 1-0 kwenye uwanja wa Uhuru. Mchezo huo ulikuwa wa tatu kwa Yanga baada ya kufungwa mechi moja na sara moja.

Zaidi Tazama Video hapa chini