Ijumaa , 25th Mar , 2016

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimewasili Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo baada ya safari ndefu kutoka D’jamena, Chad kupitia Addis Ababa, nchini Ethiopia mpaka Dar es Salaam.

Nahodha wa Stars Mbwana Ally Samatta amesema, si jambo rahisi kuweza kuiongoza timu kupata ushindi ugenini kwa mara ya kwanza akiwa Nahodha lakini anaamini ushirikiano katika mchezo huo umesaidia kuweza kupata ushindi katika mchezo wa awali.

Samatta amesema, wanasubiri maelekezo kutoka benchi la ufundi ambalo limekisoma kikosi cha Chad udhaifu wao pamoja na ubora wao ili wajue wanatumia njia gani kuweza kupata ushindi ambao utazidi kuwaongezea pointi.

Samatta amesema, timu kwa pamoja inamshikamano na ushirikiano ni mzuri ili kuweka ari ya ushindi lakini wananchi ambao ni mashabiki wa soka wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwapa sapoti katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumatatu ya Machi 28 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.