Kikosi cha zamani ya Singida United katika picha ya pamoja kilichokua na nyota bora na kutikisa nchi.
Kocha wa klabu ya Singida United,Ramadhani Nzwanzulimo amesema wameshuka daraja kutokana na changamoto nyingi kuikabili timu yao ikiwemo kuondokewa na wachezaji wengi kufuatia kutolipwa mishahara yao tangu kuanza kwa msimu huu.
Nswanzulimo ambaye aliiongoza Mbeya City kumaliza katika nafasi ya 6 msimu uliopita,amesema hata kipigo cha bao 7-0 walichokipata kutoka kwa Azam Fc,kilitokana na kutumia wachezaji wa kikosi cha nne,baada ya wale wa kikosi cha kwanza,cha pili na cha tatu kutokewa kikosini.
Kocha huyo raia wa Malawi amesema,inasikitisha kuona timu hiyo inaporomoka kutokana na viongozi kukosa mipango ya kuifanya timu ifanye vizuri,huku akigusia kukosekana kwa mshikamano baina yao.
Katika hatua nyingine kocha huyo ambaye alichukua mikoba ya Fred Felix Minziro,amesema endapo wakazi wa Singida na viongozi hawatoshikamana,upo uwezekano ndani ya miaka miwili ijayo wakakosa timu itakayoshiriki ligi kuu.
Timu ya Singida United,inaburuza mkia huku kimahesabu ikiwa imeshaporomoka daraja,ina takwimu mbovu kuliko timu yeyote katika VPL hadi sasa,kwani imefungwa michezo 24 kati ya 33,imeruhusu mabao 64 huku yenyewe ikifunga machache zaidi ambayo ni 19,imeshinda mechi 3 tu ambazo ni chache zaidi katika ligi.
Singida United ambayo rais wake ni Mh Mwigulu Nchemba chini ya mkurugenzi mtendaji Festo Sanga ilikua tishio nchini ambapo ilipopanda daraja misimi miwili iliyopita,ilifanya usajili wa kuvutia wa wachezaji wakubwa nchini na hata wa kimataifa lakini mambo yamekua tofauti tangu kuanza kwa msimu huu.
