Alhamisi , 16th Oct , 2025

‘’Wakati nilipokuwa Liverpool, nilijikuta kwenye mazingira ambayo kila mchezaji wa kweli angependa kuwa nayo klabu inayopigania mataji kila msimu, inayotawala uwanjani kwa kiwango cha hali ya juu...

lakini pia yenye roho ya kupambana hadi dakika ya mwisho. Kila siku ilikuwa ni vita, siyo kwa sababu hatukuwa na uwezo, bali kwa sababu mafanikio hayaji kirahisi  unapaswa kupigania kila bao, kila ushindi.

 

Liverpool haikuwa tu klabu niliyochezea, ilikuwa kama familia. Pale nilijifunza maana ya kujitoa, ya kuweka timu mbele kabla ya binafsi, na ya kupenda mchezo kwa moyo wote. Hapo ndipo nilipata ile mchanganyiko wa kutawala mechi, lakini pia kujua kuwa hakuna kitu kinachokuja bila kazi na kujituma.

 

Baada ya kupambana kwa miaka mingi kufikia ndoto yangu ya kuwa mchezaji wa kulipwa, na kisha kuwa mchezaji niliyetamani kuwa, hatua ngumu zaidi ilikuwa kukubali kuwa safari yangu inakaribia mwisho. Ilikuwa ngumu si kwa sababu nilikuwa na hofu ya yajayo, bali kwa sababu nililazimika kuachana na kitu nilichokipenda kwa moyo wangu wote  soka na zaidi ya yote, klabu ya Liverpool.

 

Sikuachana kwa sababu nilitaka, ila kwa sababu kulikuwa na hali zilizo nje ya uwezo wangu. Ila ndani ya moyo wangu, Liverpool itaendelea kuwa sehemu ya mimi sehemu ya historia yangu, sehemu ya ndoto zangu zilizotimia’’

 

Maneno ya Thiago Alcantara, aliyekuwa kiungo wa Liverpool, ambaye alitangaza kuondoka rasmi kwenye klabu hiyo mwaka 2024. Baada ya kipindi kizuri Anfield, Thiago alihitimisha safari yake na kurudi nyumbani kwa sasa akiwa sehemu ya benchi la ufundi ndani ya kikosi cha FC Barcelona