Kwanini Pep kamuacha Koulibaly kamchukua Ake?

Alhamisi , 30th Jul , 2020

Klabu ya AFC Bornemouth imekubali kupokea kitita cha pauni milioni 41 kutoka Manchester City ili imruhusu beki wake Nathan Ake kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya England.

Mlinzi wa kati Nathan Ake akiwashukuru mashabiki wa AFC Bornemouth ambayo imeporomoka daraja katika EPL, na sasa atajiunga na Manchester City.

 

Mkakati wa kukamilisha usajili wa beki huyo wa zamani wa Chelsea unatarajiwa kukamilika siku chache zijazo.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola ameamua kumsajili Ake na kuachana na Kalidou Koulibaly kufuatia viongozi wa The Citizen kutokua na mahusiano mazuri Napoli ambayo iligoma kuwazuia Jorginho ambaye alihamia Chelsea kipindi hiko.

Huu utakua usajili wa pili wa Manchester City kufuatia jana wababe hao kumchukua kiungo Ferran Torres kwa dau la pauni milioni 22.

KWA NINI AKE NA SIO KOULIBALY?

Kwa mfumo wa kocha Pep Guardiola, amekua akihitaji mlinzi wa kati anayetumia mguu wa kushoto ambaye mzuri kuanzisha mashambulizi ili atengeneze muungano na Aymeric Laporte kama namba 4 na 5.

Ikizingatiwa kwamba Jones Stones huenda akaondoka kikosini,huku Nicolaus Otamend anaonekana kuwa na makosa mengi, hivyo Ake ambaye hata umri wake wa miaka 24 unatoa picha nzuri ya kuwa mchezaji wa kuregemewa kwa muda mrefu, anapata kipaumbele kuliko Koulibaly ambaye ana umri wa miaka 28 na thamani yake ni kubwa .