(Nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James)
Lebron ambaye alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya misulii na ugonjwa wa tumbo amekosekana katika michezo 10 ambayo Lakers wamecheza wakishinda michezo 4 na kufungwa 6 huku Lebron akikosa michezo 8 mfululizo.
Licha ya kufanya mazoezi ya pekeeake akisimamiwa na kocha wake msimamizi, Phil Handy, lakini Lebron alishindwa kuwa sehemu ya mchezo ambao alfajiri ya leo Lakers imefungwa kwa alama 109-102 dhidi ya Mabingwa watetezi Milwaukee Bucks.
Kipigo hiko ni cha 8 kwa Lakers ambao wameshinda michezo 8 katika michezo 16 ya NBA msimu huu na kushika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa upande wa Western Conference na wapinzani wake Golden State Warriors wakiwa vinara.