Ijumaa , 13th Aug , 2021

Mchezaji mpya wa klabu ya PSG, Lionel Messi amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo ya mauzo ya jezi katika siku ya kwanza baada ya usajili.

Picha ya Mchezaji Lionel Messi

Inaripotiwa kuwa PSG tayari wameuza jezi 832,000 katika saa 24 za kwanza baada ya taratibu za kuwasili klabuni hapo kukamilika hii ikiwa imeizidi rekodi ya mauzo 520,000 ya jezi ya Ronaldo wakati anajiunga na Juventus mnamo 2018.

PSG wametengeneza kiasi cha fedha takribani Euro milioni 90 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 244.2 kwa mauzo ya jezi tu ya Messi.