Jumatano , 8th Jun , 2022

Klabu ya Liverpool ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Benifica kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Darwin Nunez (22)raia wa Uruguay kuchukua nafasi ya Sadio Mane endapo uhamisho wa mane kwenda Bayern Munich ya ujerumani ukikamilika kwenye dirisha hili kubwa la usajili.

(Nunez akishangilia baada ya kufunga bao kwenye UCL)

 

Mkurugenzi mpya wa michezo wa Liverpool, Julian Ward ndiye anayefanya mazungumzo hayo huku ikiripotiwa kuwa nyota huyo anatamani kujiunga na majogoo hao wa jiji wa nchini England kwenye msimu ujao wa mwaka 2022-2023.

 

Ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ni paundi milioni 85 za England sawa na bilioni 247 za zaidi ya milioni 211 za Kitanzania dili ambalo endapo likikamilika basi linatazamiwa litatikisa na kuingia kwenye vitabu vya rekodi barani Ulaya.

 

Nunez ambaye pia anawindwa na vilabu vya Atletico Madrid ya Uhispani na Manchester United ya England, amefunga magoli 34 na assist 4  hivyo  kuhusika kwenye magoli 38 katika michezo 41 ya michuano yote msimu uliomalizika wa mwaka 2021-2022. 

 

Nunez amemvutia Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp baaa ya kuonesha kiwango kizuri msimu uliomalizika na kuifunga Liverpool mabao 2 kwenye sare ya mabao 3-3 dhidi ya Benifica kwenye dimba la Anfield kwenye hatua ya robo fainali ya UCL.