Alhamisi , 19th Mar , 2015

Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Taifa yanatarajia kuanza kutimua vumbi hapo kesho, Uwanja wa Makongo jijini Dar es salaam kwa kushirikisha vilabu sita kutoka hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaam DRHA, Mnonda Magani amesema kwa mwaka huu vilabu shiriki kutoka mikoani havitaweza kushiriki utokana na muingiliano wa ratiba ikiwemo mabingwa watetezi wa kombe hilo ambao ni Moshi Kalsa huku timu za Magereza, TPDF wanaume na wanawake, Dar Clalsa, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na Tanzania Twende wanawake zikihakiki kushiriki michuano hiyo.

Magani amesema, mashindano hayo yanayotarajiwa kumalizika siku ya Jumapili yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kufanya mazoezi kwa bidii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo.