Alhamisi , 26th Aug , 2021

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetolea ufafanuzi juu ya nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kuwa atakuwa na kitengo maalum ambacho atafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi.

Haji Manara akiwa katika jezi mpya za Yanga

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amezima uvumi kuwa Manara ndiye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano mpya wa Yanga, jambo ambalo ilitafsiriwa kuwa .H

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amezima uvumi kuwa Manara ndiye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano mpya wa Yanga, jambo ambalo ilitafsiriwa kuwa .

''Sisi kama viongozi hatujamtangaza Manara kwamba anakwenda kubeba cheo gani, lakini watu wameunganisha kazi aliyokuwa anaifanya alikotoka, wakaamini labda anakuja Yanga kuja kufanya katika idara ile ile, lakini ukweli ni kwamba Haji Manara hajaletwa kuchukua nafasi ya mtu na hakuna kitakachobadilika.

Manara atafanya kazi na Hassan Bumbuli, na Antonio Nuggaz, tuna Mkakati kabambe na mpango wetu ni mkubwa, tunajua umahiri wa Haji namna ya kukusanya mashabiki, kwa wale wenye mashaka ipo siku watatuelewa''Haji Mfikirwa akizungumza na East Afrika Radio.

Katika hatua nyingine Mfikirwa amesema huku ya kesi baina yao na mchezaji Benard Morrison ,bado haijatolewa na Mahakama ya Usuluhishi Michezoni CAS hivyo na wao wanasubiri majibu yake hivyo Wanachama wanapaswa kuwa wavumilivu.