
Kiungo wa Totenham Hotspurs Delle Ali akifunga bao la kwanza kwa timu yake huku mlinda mlango wa Manchester United Davuid de gea akiwa hana la kufanya.
Klabu ya Manchester United huenda ikakabiliwa na adhabu kutoka kwa chama cha soka nchini Uingereza kufuatia klabu hiyo kuchelewa kuwasili jijini London uwanjani White Hat Lane kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Totenham Hotspurs hapo jana.
Awali mechi hiyo ilipaswa ichezwe saa 12 kamili lakini ikasogezwa mbele kwa dakika 15 lakini ikaanza dakika 30 baadae kutokana na gari la kikosi cha mashetani wekundu wa jiji la Manchester kuchelewa kuwasili kutokana na foreni kubwa iliyosababibishwa na barafu kujaa barabarani.
Kutokana na Sheria la ligi kuu nchini humo kwa timu itakayochelewa kwa dakika 15 au pungufu ya hiz italazimika kulipa faini ya pauni elfu tano lakini kwa Manchester watalazimika kusubiri uamuzi wa FA kwa kuwa wao walichelewa kwa zaidi ya dakika hizo.
Katika mchezo huo Manchester United ilikubali kipigo cha mabao 3-0 ambacho ni cha kwanza tangu mwaka 2001 katika uwanja huo lakini pia kimekwamisha jitihada za timu hiyo kumaliza katika nafasi nne za juu za ligi.
Hii si mara ya kwanza katika uwanja wa White Hartlane kwani hata msimu wa 2012/13 ilitokea tena mechi ya Tottenham na Man united kuchelewa kwa dakika 15 .