Jumanne , 10th Sep , 2019

Shirikisho linalo simamia mchezo wa Kikapu Amerika Ya Kaskazini (NBA), imetaarifu mpango wake wa kupiga marufuku uvaaji wa vitambaa kichwani (Headbands) kwa staili ya kininja kwa msimu unaokuja wa mwaka 2019-20.

Mchezaji Karl-Anthony Towns wa Minnesota Timberwolves.

Hayo yameelezwa na mkuu wa idara ya mawasiliano wa NBA, Mike Bass kuwa uvaaji wa staili hiyo haujawahi kuwa aina ya uvaaji unaokubalika katika mashindano yao pia ni ukosefu wa weledi.

"Wachezaji walipoanza kuvaa msimu uliopita tulishindwa kukataza ili kuepuka mkanganyiko lakini tuliwataarifu tangu mwezi Mei kwamba aina hiyo ya uvaaji haitatumika tena katika misimu inayofuata," alisema.

Timu kadhaa zimeomba utaratibu huo mpya uwashirikishe na wao pia hususani kwa kuangalia katika matumizi ya usalama, urefu, aina ya uvaaji na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa na usaidizi kwa wachezaji.

Wachezaji kama Jimmy Butler, Jarret Allen, Jrule Holiday, Karl-Anthony Towns hata Lebron James ni mojawapo ya wavaaji wakubwa wa staili hiyo ambao kwa msimu unaokuja huenda tusiwaone tena na kitu chochote katika vichwa vyao.