
Kocha mpya wa RB Leipzig Jesse Marsch
Jesse Marsch Mmarekani mwenye umri wa miaka 47 alikuwa anafundisha klabu ya RB Salziburg ya Austria amepata nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha wake Julian Nagelsmann kujiunga na Bayern Munich mwisho wa msimu huu.
Mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo Oliver Mintzlaff amesema, ''tumelazimika kuajiri kocha mkuu kwa haraka kwa kuwa ni nafasi muhimu katika maendeleo ya klabu, tunapenda kufanya kazi na makocha wa kiwango cha juu kama alivyo Jesse Marsch''.
''Kwetu sisi ni faida kubwa sana kumpata kocha tuliyewahi kufanya naye kazi, Marsch aliwahi kuwepo hapa kama kocha msaidizi hivyo anaifahamu klabu,analifahamu jiji la Leipzig na filosofi ya timu yetu'' aliongeza Mintzlaff.
Marsh aliyejiunga na klabu ya RB Salzburg june 2019, ameiongoza timu katika michezo 89 ameshinda michezo 59 sare13 anepoteza michezo 17 amefanikiwa kufunga magoli 273 na kufungwa magoli 110 anaichukua RB leipzig ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo kwa wakati huu.