Jumapili , 6th Mar , 2022

Takriban Mashabiki 22 wamejeruhiwa kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Mexico (Liga MX) katika mchezo baina ya klabu ya Queretaro dhidi ya klabu ya Atlas kwenye uwanja wa La Corregidora Jumamosi ya Machi 05, 2022.

(Mashabiki waliovamia uwanja na kuanzisha vurugu)

Polisi nchini humo imethibitisha watu wawili kujeruhiwa vibaya huku watu tisa wakipelekwa hospital baada ya kutokea vurugu uwanjani zilizosababishwa na mashabiki kuvamia eneo la kuchezea na kuanzisha mapigano, huku baadhi ya wachezaji wakifanya jaribio la kuwasihi mashabiki kuacha vurugu lakini ilishindikana na kisha kutolewa uwanjani na kwenda vyumbani.

(Mashabiki waliovamia kwenye uwanja wa La Corregidora katika ligi kuu ya mexico)

"Kwa ajili ya heshima ya watu waliopata majeraha,tumehairisha michezo ya jumapili na wote waliozembea kwenye suala la ulinzi na kupolekea ukosefu wa usalama watashughulikiwa "alisema Mikel Arriola ambaye ni rais wa bodi ya ligi kuu nchini Mexico.

Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 63 huku wageni klabu ya Atlas walikuwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Queretaro.