
Obrey Chirwa
Taarifa iliyotolewa jana na Yanga ilisema wachezaji Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu hawatafuatana na timu hiyo kutokana na sababu mbalimbali.
Kufuatia taarifa hiy baadhi ya mashabiki wa Yanga walianza kuhoji kutaka kujua ni sababu zipi zilizopelekea Chirwa kutoongazana na kikosi hicho, huku wakitaka kufahamishwa au kuwekwa wazi ili wajue kama ni majeraha au lah, lakini tetesi zilizopo mtaani ni kwamba mchezaji huyo amegoma kuondoka na kikosi hicho kufuatia kutolipwa mshahara wake kwa miezi kadhaa.
Kufuatia kuzuka kwa tetesi hizo wapo mashabiki wa Yanga ambao wameonesha kuumizwa na kitendo alichofanya mshambuliaji huyo na kusema kuwa wao walimvumilia kipindi ambacho alikuwa akifanya vibaya, lakini imefika kipindi anafanya vyema ameanza kuleta dharau na kushindwa kuwavumilia katika kipindi hichi.
Kikocho cha Yanga
"Huyu f*** Chirwa tulimvumilia tukampa nafasi tukamwacha kipenzi cha wana Yanga Mbuyu Twite kisa tukimpa nafasi. Aondoke hatumuhitaji na wale wazee waliokimbilia mahakamani na kwa Mkuu wa Mkoa wako wapi wasilipe mishahara au walikuwa wanatetea matumbo yao....Nimekasirika sana mpaka nalia":- Boll Mlingi Bull Mlingi
Mashabiki wameendelea kulalamika juu ya jambo hili kutokuwa wazi
"Mbona hamtoi taarifa iliyonyooka sababu mbalimbali ndiyo nini mfano Obrey Chirwa tulipaswa kujua ni majeruhi au ana kadi? Mchezo wa soka wa leo taarifa zinatakiwa ziwe wazi wapenzi tujue acheni kutuachia maswali" aliandika Taleeb Zaramo
Mbali na hao mashabiki wengine wengi wa Yanga wameitakia mafanikio mema timu yao huku wakiwataka wachezaji kujitahidi kujituma na kucheza kwa kujiamini ili waweze kushinda mchezo huo wa marudiano.
Haya ndiyo maoni yao