Jumamosi , 10th Jun , 2017

Land Force imekuwa timu ya kwanza kutolewa katika michuano ya Sprite BBall Kings baada ya kuchapwa na Dream Chaser kwa 'point' 92-72 katika hatua ya mtoano, ambapo mchezo huo umepigwa katika uwanja wa Air wing, Ukonga Jijini Dar es Salaam mapema leo.

Dream Cheaser na Land Force ndizo zilikuwa timu za awali katika kufungua duru la mtoano ya michuano hii huku mchezaji Gwakisa Mwasakyeni kutoka Land Force ameibuka 'best scorer' kwa pointi 40 akifuatiwa mpinzani wake Jovin Charles kutoka Dream Cheaser kwa kupata pointi 39 katika mechi ya kwanza.

Timu ya Dream Chaser

Mshindi wa mashindano haya ataweza kuibuka na kitita cha Milioni 15 pesa taslimu za kitanzania huku mshindi wa pili kuondoka na Milioni tatu na kumaliziwa na mchezaji bora 'Most Valuable Player' kuondoka na Milioni mbili.

Timu ya Land Force

Katika mtanange wa Dream Chaser na Land Force umechezeshwa na refa Edwin Kilagwa pamoja na msaidizi wake 'Empire'  Faraja Jime, mchezo wa mtoano kwa timu zingine  unaendelea.