
(Bingwa mpya wa Langalanga 2022 Dereva Max Verstappen)
Max Verstappen raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, Ametwaa ubingwa huo ikiwa ni mara ya pili baada ya kutwaa msimu uliopita wa mwaka 2021 huku akimzidi dereva mwenzake wa Red Bull Sergio Perez alama 113 anayeshika nafasi ya pili akiwa na alama 253 huku zikisalia mbio 4 kumalizika kwa msimu wa mwaka 2022
Kwenye mbio za Japan Grand Prix 2022,nafasi ya pili imechukuliwa na Dereva wa Red Bull huku Dereva Charles Leclerc akimaliza nafasi ya tatu ilhali Dereva Esteban Ocon akishika nafasi ya nne huku Muingereza Lewis Hamilton anayeendesha kampuni ya Mercedes akimaliza nafasi ya tano.