Jumamosi , 2nd Sep , 2017

Mchenga BBall Stars wamefanikiwa kuwachapa wapinzani wao TMT kwa pointi 102-94 mchezo wa tano na wa mwisho katika fainali za Sprite BBall Kings uliyopigwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.

Timu ya Mchenga BBall Stars wakiwa pamoja na Afisa Masoko msaidizi wa kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge (aliyevaa t-shirt ya blue).

Kutokana na matokeo hayo timu ya Mchenga BBall Stars imeweza kuwa mabingwa wa Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017 na kuweza kuchukua kile kitita cha Milioni 10 kama zawadi ya mshindi wa kwanza pamoja na kikombe chake huku TMT ikiangukia nafasi ya pili na kuchukua zawadi ya Milioni tatu.

Timu ya TMT ikiwa imeshikilia mfano wa hundi wenye thamani ya Milioni tatu baada ya kushinda nafasi ya pili michuano ya Sprite BBall Kings 2017.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweze kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kupania kuwa bingwa jambo ambalo lilipelekea timu hizo kujikuta zikitoka sare ya pointi 84-84 kwa mara ya kwanza na kupelekea waamuzi kulazimika kuongeza dakika nyingine tano ili aweze kupatikana mshindi wa mashindano hayo na ndipo Mchenga BBall Stars alipomchapa TMT jumla ya pointi 102-94

Kwa upande mwingine, mchezaji Rwahabura Munyagi kutoka timu ya Mchenga BBall Stars ameweza kushinda nafasi ya mchezaji bora 'MVP' kwa kuweza kuipigania timu yake kushinda mchezo wa leo.
 

Rwahabura Munyagi aliyeshinda nafasi ya mchezaji bora 'MVP' katika michuano ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017.