Jumatatu , 21st Jan , 2019

Mcheza tenisi, Roberto Bautista Agut ambaye hivi sasa yupo kwenye robo fainali ya michuano ya wazi ya Australia, ameweka wazi kuwa alipenda zaidi soka kuliko tenisi na aliwahi kucheza katika klabu ya Virrareal ya Hispania.

Roberto Bautista Agut

Roberto Bautista amefanya mahojiano maalumu na runinga ya ligi kuu ya Hispania La Liga na kueleza kuwa ilimbidi kuchagua tenisi kutokana na yeye kupewa nafasi zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu japo aliupenda sana.

"Nilipokuwa mtoto nilikuwa nakwenda kwenye uwanja wa El Madrigal kuangalia Villarreal kwasababu nilitaka kuwa mcheza soka na nilianza kucheza hapo mpaka nikiwa na miaka 14 ikanibidi kuhamia kwenye tenisi maana nilijitahidi kufunga hata kwa masikio yangu lakini sikupata muendelezo", amesema.

Roberto ambaye anashika namba 24 kwa viwango vya tenisi duniani kwa upande wa wanaume kesho atakutana na Stefanos Tsitsipas wa Ugiriki kwenye robo fainali ya michuano ya wazi ya Australia.

Roberto mwenye miaka 30, ambaye ni bingwa mara 9 wa ATP Tour, amesema moja ya klabu za soka alizozichezea katika maisha yake ya utotoni ni CD Castellon ambayo ni timu ndogo pale mjini Virrareal na walicheza nguli kama Vicente del Bosque and Gaizka Mendieta.