Jumatano , 15th Apr , 2015

Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Zanzibar, Mcha Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Khamis Mcha Viali

Baba huyo wa kiungo wa Azam FC na Timu ya Taifa Stars, Khamis Mcha Viali amefariki dunia jijini Dar es salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake, Mcha alichezea Klabu za KMKM na Miembeni pamoja na Timu ya Taifa ya Zanzibar.