
Lionel Messi
Messi ameyasema hayo wakati anafanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni kiitwacho 'La Sexta' hii leo nchini Uhispania na kugusia mambo mengi ikiwemo suala la uhamisho wa mshambuliaji mwenzake Luis Suarez kuhamia Atletico Madrid na hatma yake kiujumla.
Messi amesema “Sikupenda jinsi alivyoondoka. Sifikiri kama amestahili kuondoka namna ile. Amelipia sehemu ya mkataba wake uliobakia mbaya zaidi ameenda upande ambao unashindania kitu kimoja na sisi”.
Kuhusu suala la hatma yake klabuni hapo, Messi amesema, “Nimesema sikuzote kwamba ningependa kupata changamoto katika ligi kuu ya nchini Marekani lakini sio kwasasa. Na hata ikitokea nimeondoka nataka niondoke kwa mahusiano mazuri zaidi”.
Messi amesisitiza kama akiondoka anagependa aondoke vizuri kwasababu amekiri kuwa na malengo ya kurejea kuhudumu kwenye klabu ya Barcelona iliyomlea kwa muda mwingi na kumpa nafasi ya kuwa mchezaji bora Duniani.